Baada ya kutoa Cash money kinachofuata ni kurudishiwa chenji,Muuza samaki akiwa na mteja wake ambaye ananunua samaki kama kitoweo cha nyumbani,Wafanyabiashara kama hawa wangejengewa sehemu mahususi kwa kazi hizi na kuwekewa hali na mazingira ya usafi kwa afya za walaji lingekuwa jambo la msingi sana kuliko kuuza sehemu zenye uwazi na vumbi.
Msichana mdogo mwenye umri wa kwenda shule akiwa mtaani kutafuta riziki ya wanafamilia kwa kuuza korosho.Je kuna hathari gani kwa msichana kama huyu kuuza korosho? Anapungukiwa nini kwa kutokwenda shule? Tutegemee nini kwa mtazamo kama huu?