Wachezaji wa timu ya Uganda wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe lao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Ali Mohamed Shein akikabidhi kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 kwa wachezaji wa timu ya Uganda (The Cranes) mara baada ya timu hiyo kushinda kombe hilo kwa kuifunga timu ya Rwanda (Amavubi) katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam.
Ilikuwa ni fainali ya kuvutia kwa timu zote mbili kutokana na kiwango kilichoonyeshwa katika dakika 90, timu hizo zilitoka suluhu ya magoli 2-2 ambapo dakika 30 ziliongezwa lakini hazikuzaa matunda kwa timu zote mbili, mpaka ilipofika wakati wa mikwaju ya penati, timu ya Uganda ilipata penati 4-3 dhidi ya Rwanda, hivyo Uganda kutawazwa mabingwa wapya wa kombe hilo.(Kwa Ihsani ya FULL SHANGWE)