Timu za wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania za wanawake na wanaume zikiwa katika picha ya pamoja na vikombe vyao mara baada ya kushinda michezo yao na kuzifunga timu za baraza la Wawakilishi Zanzibar katika mpira wa miguu na netiboli, katika michezo iliyofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana. Michezo hiyo ilikuwa ni kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, ambapo katika netiboli timu ya wanawake iliifunga Baraza la Wawakilishi na Timu ya wanaume katika mpira wa miguu iliifunga Baraza la Wawakilishi magoli 4-1 na kuibuka kidedea huku mfungaji bora wa mchezo huo akiwa Mh. Adam Malima. Timu hizo za Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na ili ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar zilidhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) 
Duuh kweli Tanzania kuna vipaji..Ebu ona Muheshimiwa William Ngeleja alivyomtoka mmoja wa walinzi wa Baraza la wawakilishi na jinsi anavyoonekana katika Motion utasema ni mmoja wa wachezaji hatari wa Manchester United au Dar Young African ya Jangwani jijini Dar es Salaam,hii picha nimeipenda sana kiukweli.Wabunge waliibuka washindi baada ya kuibanjua timu ya Baraza wa Wawakilishi kwa jumla ya magoli 4 - 1. (Picha kwa Ihsani ya full shangwe).