Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua baiskeli ya miguu mitatu iliyotengenezwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) kwa ajili ya walemavu na ambayo baada ya kuikagua alishauri ifanyiwe majaribio kabla ya kuzalisha nyingi.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mike Laizerna kushoto ni Meneja wa SIDO wa Mkoa wa Dar es salaam, Hamwel Meena na wapili kushoto ni Ofisa wa Ufundi wa SIDO, Mina Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)