UCHUMBA wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Jumaa ‘Diamond’ na Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, umekucha tena licha ya shutuma za Wema kwa mlimbwende Jokate Mwegelo kwamba alimkuta akiwa ‘kihasarahasara’ na mpenzi wake huyo, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Hata hivyo, mara baada ya madai ya Wema, Desemba 10, mwaka huu, Diamond alipanda ndege kwenda London, Uingereza kwa mkataba wa kutumbuiza shoo kadhaa.
AHOJIWA UINGEREZA KWA DAKIKA 30
Akihojiwa kwa dakika 30 na mtangazaji Miss Justina George katika Live Talk Show ya AILTV nchini humo, nyota huyo alishindwa kuweka wazi kwamba, alitoka Bongo akiwa ametuhumiwa kusaliti, badala yake akasema ana mchumba (Wema) ambaye anampenda kupita maelezo.

RISASI LAMWENDEA HEWANI LONDON
Akizungumza na paparazi wetu kwa njia ya simu akiwa London Desemba 16, mwaka huu, Diamond alisema baada ya kumaliza shoo zake nchini humo angerejea Bongo na bonge la ‘sapraizi’ kwa Wema.
Alipoambiwa huku Bongo, Wema amekuwa akitangaza kummwaga baada ya kudaiwa kukutwa sirini na Jokate, Diamond alijibu:
“Hakuna kuachana hapa, Wema bado ni mchumba wangu, nampenda sana.”

AREJEA BONGO, AWEKWA ‘MTUKATI’

Desemba 21, mwaka huu, Diamond alirejea Tanzania, asubuhi ya Desemba 22, gazeti hili lilimtwangia simu na kutaka kujua uchumba wake na Wema umefikia wapi baada ya yeye kutua Bongo.
Diamond: “Nimerudi jana, Wema mzima sana.”
Risas Jumamosi: “Oke, uko naye hapo au?”
Diamond: “Hapana.”
Risasi Jumamosi: “Kumbe kweli mmemwagana?”
Diamond: “Sijamwagana na Wema.”
Risasi Jumamosi: “Yaani kama si kweli, iweje urejee Tanzania ushindwe kuonana na mchumba‘ako?”
Diamond: “Kweli kabisa hatujamwagana, nipo naye.”
Risasi Jumamosi: “Nipe niongee naye.”
Diamond: “Mimi kuna sehemu nakwenda, nimemwacha kitandani hajaamka.”
Risasi Jumamosi: “Kwa hiyo mambo mmemaliza?”
Diamond: “Tuko sawa kabisa.”

WEMA VIPI?
Baada ya kuzungumza na Diamond, Risasi Jumamosi lilifanya juhudi za kumpata Wema kwenye simu, lakini kilongalonga chake kiliita kwa muda mrefu na mara bila kupokelewa.
Hata pale alipotumiwa ‘SMS’ na kujulishwa kila kitu, hakujibu hadi tu nakwenda mitambo.                           CHANZO CHETU CHA HABARI NI HAPA