Baada ya kuona wasambazaji wa Filamu wengio ni mizingua na hujinufaisha wao zaidi ya Msanii hwa jamaa wa MIZENGWE ambao ni manguli wa vichekesho pale ITV wameamua kuingia mtaani wao wenyewe na kufanya umachinga wa kuuza filamu yao.
Wasanii hao kadha mbali na kufanya vyema katika vichekso vya kwenye Luninga pale ITV pia wameunda kundi lao linalojulikana kama KASHA KASH.
Mara kadhaa wamekuwa wakionekana katika mikusanyiko ya watu wakiuza filamu yao hiyo na jana walibahatika kunasa wao wenyewe mbele ya Camera ya FK BLOG na hatimaye kupata taswira hizi wakiwa katika Viwanja vya Julius Nyerere almaarufu Sabasaba pale barabara ya Kilwa wakiuza Filamu yao hiyo ya Kash Kash kwa watu waliofika kuangalia maonesho ya miaka 50 ya Uhuru.(Na FK)