Hello wapenzi na wasomaji wa Maganga One Blog.
Napenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha kuwa leo mimi na mke wangu tumejaaliwa kupata mtoto wa kike katika hospital hiyo hapo pichani hapa Ulaya.Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia neema hii.

Furaha niliyonayo inamzidi mke wangu ambaye bado yupo kwenye mjengo huo pichani (hospital) kwa uangalizi zaidi,amejifungua salama na kwa njia ya kawaida bila matatizo yoyote ila kama ilivyo utaratibu hospitali za wenzetu lazima ukae japo siku nne kwa uangalizi wa hali yako na mtoto wako.

Kwa taarifa hii fupi napenda kuwaomba wapenzi wangu na wasomaji wangu ruksa ya likizo fupi ili nijidaidai na wife na mtoto wetu mpya.Hivyo basi naomba mjue nitakuwa bize kidogo na mtoto mpya na hivyo shughul za Blog zitakuwa zikiyumba kidogo kwa muda usiojulikana.Nategemea kueleweka vilivyo na nawatakia kila la heri katika siku ya leo na zijazo.
                                           Maganga One.