Wasanii wa Bendi ya PGN inayopiga muziki wa Injili wakiimba na kucheza jukwaani.
SSP wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Eva Stesheni akitoa somo la ujasiriamali.
Mkurugenzi wa UGM, Emmanuel Ezekiel akisikiliza somo la ujasiriamali lililokuwa likitolewa na Eva Steshen.
     Vikundi mbalimbali vya burudani na vyuo vilishiriki katika kongamano hilo.
Msanii maarufu nchini, Masanja Mkandamizaji pia alihudhuria katika kongamano hilo.
Mlezi wa GMC, Pastor Salome Mramba akitoa neno ukumbini hapo.
7. Hiki ndicho kikosi kamili kilichoandaa kongamano hilo kutoka GMC kinachoongozwa na Pastor Salome
8. Waliohudhuria kongamano hilo wakimuomba Mungu ili kulibariki kongamano hilo lianze na kwisha kwa amani.
9. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP David Misiime pia alihudhuria katika shughuli hiyo.
10. Mratibu wa Burudani wa Ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo akiteta jamabo na Masanja.

MWISHONI mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa kisasa wa burudani wa Dar Live uliopo Zakhem, Mbagala jijini Dar es Salaam kulifanyika kongamano lililohusu ujasiriamali kwa polisi shirikishi lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kundi la GMC linaloongozwa na Pastor Salome Mramba.
Pamoja na mambo mbalimbali yaliyojiri siku hiyo, Bendi ya UGM inayopiga muziki wa Injili ilikonga vilivyo nyoyo za waliohudhuria kwa vibao vyake kadhaa.
Mrakibu wa polisi kutoka Mkoa wa Kipolisi Temeke, Eva steshen (SSP) ndiye alikuwa akitoa somo la ujasiriamali katika kongamano hilo ambapo waliohudhuria walilishuru jeshi hilo kuwapa elimu ya biashara ambazo wanaweza kuzifanya kwa kutumia mitaji waliyonayo.
Akizungumza katika kongamano hilo, mlezi wa Kanisa la GMC, Pastor Salome Mramba ambaye alikuwa miongoni mwa waliotoa mafunzo ya ujasiriamali alisema bila kumuogopa Mungu mambo hayawezi kwenda , aliwaasa watanzania wawe na mioyo ya kumuogopa Mungu kwa maana hiyo tunaweza kupambana na kila kitu ikiwemo kupunguza maambukizi ya Ukimwi , watu kuibia serikali mapato mbalimbali kwa kutumia neno ufisadi.

                                            (Habari, picha na Haruni Sanchawa wa GPL)