Kesi dhidi ya wasomali saba wanaoshtakiwa kuwa maharamia imeanza nchini Malaysia.
Ni kesi ya kwanza kuhusu watu wanaoshukiwa kuwa maharamia kufanyika barani Asia.
Wasomali hao walikamatwa na wanajeshi wa ulinzi wa bahari nchini humo mwaka jana baada ya njama yao ya kuteka meli ya mafuta katika ghuba ya Aden kutibuka.
Wanatuhumiwa kwa kuwafyatulia risasi makomando wa baharini Malaysia kwa lengo la kuwajeruhi. Watahukumiwa kifo ikiwa watapatikana na hatia.
Mahakama ya juu mjini Kuala Lumpur inasema kuwa ina haki kutoa uamuzi licha ya tukio la shambulizi kutokea mbali sana na nchi hiyo katika bahari kati ya Yemen na Somalia.