Mkuu Wa Mkoa Wa Iringa,Awataka Wananchi Kuzingatia Sheria Za Barabarani
 Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dk.Christine Ishengoma akisalimiana na maofisa wa polisi
Mkuu wa mkoa wa Iringa akipata maelekezo katika banda la kampuni ya simu ya 'Air tel'
Mkuu wa mkoa wa Iringa, akisikiliza maelezo ya namna ya kutumia alama za barabarani,kutoka kwa mtoto wa shule ya msingi
Waendesha pikipiki (bodaboda)
Mkuu wa mkoa wa Iringa,Dk.Christine Ishengoma amewataka wananchi na wadau wengine wa barabara,kuzingatia sheria za barabarani,ili kuepusha ajali zisizo kuwa za lazima.
Akikagua mabanda mbalimbali kwenye maadhimisho ya wiki ya 'Nenda kwa usalama barabarani' ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Iringa,mkuu huyo wa mkoa amesema,ni vizuri wananchi,madereva na watembea kwa mguu wakazingatia alama hizo ili kuepusha ajali.