Tume ya Umoja wa mataifa inayochunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Syria, imekusanya majina ya washukiwa vitendo vya uhalifu wa kivita nchini humo.
Wachunguzi wa tume hiyo wanawashutumu wanajeshi wa serikali kwa kuhusika katika uhalifu wa kivita.
Ripoti hiyo ni mojawapo ya ripoti zinazoikosoa zaidi serikali ya Syria kuwahi kupokelewa na Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa tume hiyo Paulo Pinheiro, alisema kuwa lina ushahidi wa kutosha kuhusiana na madai hayo.


Alisema kuwa ana orodha ya majina ya washukiwa wakuu wa uhalifu wa kivita na kutaka Umoja wa mataifa kuwasilisha kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Syria kwa Umoja wa Mataifa.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa baraza hilo la haki za binamu kuchukua hatua.

Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za kibinadamu la Huma Rights Watch, limesema kuwa lina ushahidi wa kuthibitisha kuwa waasi nchini syria wamewatesa mateka mbali na kuwauwa wengine.

Shirika hilo ilikusanya ushahidi mwezi jana wa mauaji na mateso dhidi ya mateka yanayotekelezwa na upinzani katika mji wa Allepo na maeneo jirani .

Ripoti ya shirika hilo inalenga madai ya mauaji ya watu wanne wa familia moja na vuguvugu la Free Syrian Army.

Human Rights Watch linasema kasi ambapo watu hao waliuwawa inafanya madai ya upinzani kuwa walitendewa haki kuwa urongo mtupu