Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania Albert Makoye akifungua mashindano ya Redd's Miss Kinondoni Talent, pembeni yake ni Ssebo ambaye ni mmoja kati ya mwanabodi wa Redd's Miss Kinondoni 2012 na alikuwa ni mshereheshaji katika shindano hilo lililofanyika katika hoteli ya JB Belmonte, iliyopo jengo la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mshiriki namba 6, Irene akionyesha manjonjo yake katika kucheza.

Mshiriki namba 3, Nahma Saidi yeye aliambua kuonyesha mambo ya Pwani.

Mshiriki namba 2, Ester Musa alionyesha kipaji cha kuimba.

Mshiriki namba 4, Diana Hussein akionyesha jinsi ya kubuni vazi.

Brigitter Alfred mshiriki namba 9 alionyesha umahili wake katika nyimbo za kihindi.

Wakiwa katika nyuso za furaha ni warembo walioshinda katika Kinyang'anyiro cha Redd's Miss Kinondoni Talent kutoka kulia ni Judith Sangu, Brigitter Alfred na Diana Hussein. Warembo hao wamepatiwa zawadi ya kupewa huduma Perfect Lady Saloon kwa kila mmoja kipindi cha Mwaka mzima.