Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa jukwaani.STAA wa muziki na filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amesema suala la kuripotiwa kuwa wanavaa utupu linasababishwa na baadhi ya watu wanaopenda kuwachungulia wasanii wanapokuwa jukwaani na kuwapiga picha.
Akizungumza na Mbovumbovu za Mastaa, Shilole amesema watu hao wanatabia ya kuwachungulia kwa chini huku ‘wakiwafotoa’ picha na ndiyo chanzo cha matatizo mengi ya skendo zinazopamba magazeti kila kukicha.
“Yaani hili nimelishuhudia kwa macho yangu mtu anakuchungulia kwa chinichini halafu akikuotea vizuri ndiyo madhara yanakuwa makubwa kama tulivyoona kwa baadhi ya mastaa,” alisema
Shilole.