Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mafundi na wahandisi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya Nyaza Road inayojenga kwa kiwango cha lami barabara ya Pansiasi Buzuruga wakati alipoweka jiwe la misngi la ujenzi wa barabara hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Septemba 16, 2012.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Ilemela wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipoweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Barabara ya Pansiasi Buzuruga kwa kiwango cha lami akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza, Septemba 16, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru Mbunge wa zamani wa Busega, Raphael Chegeni ambaye alichangia shilingi milioni moja katika harambe ya kuchangia ujenzi wa Kanisa Katoliki la Pansiasi wilayani Ilemela Septemba 16, 2012. Zaidi ya Shilingi milioni 70 zilichangwa katika harambee hiyo. 
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha Bujora wilayani Ilemela wakicheza ngoma ya Bugobogobo wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mgomeni, Kirumba, akiwa katika ziara ya mkoa Mwanza , septemba 16,2012. (Picha na Ofisi a Waziri Mkuu).