Waziri Mkuu, Mizengo Pinnda na Mkewe Tunu (kushoto) wakivuka katika Pantoni ya MV Ujenzi kutoka Kisorya hadi Rugezi Ukerewe wakiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Septemba 11, 2012. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina.

Wasanii wakitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Getreude Mongella mjini Nansio akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza, Septemba 11, 2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Viongozi wa Wilaya ya Ukerewe baada ya kuwasili Mjini Nansio kwa ziara ya kikazi Septemba 11, 2012. Kushoto ni Mkuu wa WIlaya hiyo, Mary Tesha.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu