Msanii maarufu nchini Tanzania  Kutoka kundi la Orijino Komedi al maarufu kama Mpoki (a k a Muarabu wa Dubai) anatarajiwa kuondoka nchini mapema mwanzo wa wiki hii kuenda nchini Ujerumani kwa ajili ya kuhudhuria  Mkutano mkuu wa Umoja wa Watanzania Ujerumani (U T U), utakaoambatana na Kongamano la kibiashara pamoja na Sherehe za Muungano wa Tanzania , zitakazoanza  siku ya ijumaa tarehe 25.04.14 na kumalizika siku ya Jumamosi Tarehe 26.04.14.

Akiongea na vyanzo vyetu vya habari msanii huyo alisema kuna umuhimu mkubwa wa safari yake ni  kuwakilisha wasanii wa Tanzania katika Tamasha hili kubwa  la aina yake, aidha aliendelea  kufafanua  kuwa wakati umefika kwa wasanii wa Tanzania kushirikiana kikamilifu na Watanzania wanaoishi nje ya nchi ili kuweza kupata fursa mbali mbali  zilizopo nje ya Tanzania, aliendelea kwa kusema  amevutiwa sana na Umoja Wa Watanzania Ujerumani (U T U) kwa shughuli zake   mbali mbali ambazo umekwishazifanya nchini humo  na ameamua kutoa mchango wake wa hali na mali kuhakikisha     (U T U) inafanya vizuri zaidi katika shughuli  zake mbali mbali. Ameongeza kwamba yeye binafsi amekuwa ni mfuatiliaji wa karibu sana  wa shughuli za umoja huo.

Akiongea na vyanzo vyetu vya habari Mwenyekiti  wa Umoja Wa Watanzania Ujerumani U T U Bw. Mfundo Peter Mfundo alithibitisha kwa safari ya msanii huyo Maarufu nchini Tanzania. Alisema U T U Ilipendelea sana wasanii zaidi kuhudhuria sherehe hizi lakini kwa bahati mbaya  haikuwezekana  kutokana na mambo yalio nje ya uwezo wa  U T U, aidha  U T U  ni chombo kinachokubali sana na kuzifagilia kazi za wasanii wa Tanzania.

U T U inamtakia Bw Mpoki Safari njema.