Mwanabalozi wa Zimbabwe nchiniNigeria ameitwa akajieleze kwa sababu ya matamshi ya Rais Robert Mugabe kuhusu rushwa.
Mwezi uliopita Rais Mugabe alilalamika kuwa Wa-Zimbabwe wanaanza kuwa kama Wa-Nigeria - wakitaka jambo lifanyike inabidi watie mkono mfukoni.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Nigeria imemwambia balozi wa Zimbabwe, Stanley Kunjeku, kwamba hawakubali shambulio hilo la kuwatusi.