Vijana hawa pichani majina yao hayakuweza kupatikana kwa haraka,wakiwa wanaomba msaada wa kuachiwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuwapa mkon'goto wa ajabu alfajir ya leo baada ya kushindwa zoezi lao la kuvunja na kuiba sehemu za Sinza jijini Dar es Saalam.
Kelele za kuomba msamaha zilitawala kwa vijana hawa ila wananchi wamechoka kurudishwa nyuma na wezi..wezi wabaya sana kwa maendeleo ya wananchi.

Hali mbaya ni damu kila sehemu za mwili kwa vijana hawa,wananchi wanapiga wanavyotaka wao,hakuna wa kuwaonea huruma kwa tabia zao za kuwaibia 

 Ooooh hapa sasa hawajiwezi kabisa,kichapo ni kikali na jamaa wanaonyesha kukata tamaa kabisaa,huku mmoja wapo akiwa hajiwezi tena,kweli za mwezi ni arobaini
 Kwa msaada wa polisi kufika eneo la tukio vijana hao walijikuta wananusurika kufa..mpaka vijana wanaleta habari hii mtamboni vijana walikuwa wakiendelea kupumu{walikuwa hai} ila kipigo kilikuwa heavy kwao.
Tukio hili limetokea leo majira ya saa kumi na mmoja asubuhi maeneo ya sinza kumekucha maarufu kwa jina la DR cool production. Wezi hao walitaka kubomoa duka bila mafanikio ndipo walipokamamatwa na kujitahidi kukimbia huku wakijikuta wameshakamatwa kutokana wingi wa watu walio kuwa wakiwahi makazini muda huo, hadi tunatoka eneo la tukio wezi hao walipelekwa kituo cha polosi huku wakiwa wazima japo wameshapigwa sana na wananchi. Pichani polisi taratibu wakiwapeka sehemu husika vibaka hao...