Tubingen,Ujerumani.

Mwanamuziki maarufu wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka
Bagamoyo,Tanzania,anatarajiwa kupanda jukwaani katika maonyesho makubwa ya kimataifa ya 5th.International African festival Tubingen 2014,nchi ujerumani.
Mwanamuziki huyo nguli wa reggae amepewa nafasi ya pekee ya kutumbuiza mara mbili kwa siku tofauti katika viwanja vya onyesho hilo Festplatz,Europa str. mjini Tubinge kusini mwa ujerumani, ambako maonyesho yatafunguliwa 17.julai 2014 hadi 20.Julai 2014,maonyesho ya Tubingen yategemewa kukusanya umati wa watu zaidi ya 100,000 na yanazishirikisha bendi na wasanii mbali mbali wa nchi za kiafrika.Pia
Mabalozi na wawakilishi wa nchi mbali mbali za kiafrika wameshaanzakuwasili katika mji huo wa Tubingen ,kuudhuria maonyesho hayo.