Wazazi wa wasichana waliotekwa nyara Nigeria
Wazazi wa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wamekataa wito wa kukutana na rais wa taifa hilo Goodluck Jonathan.
Hakuna sababu zozote zilizotolewa na wazazi hao.

Baadi wanamkosoa rais Goodluck kwa uamuzi wake wakisema umeshinikizwa na Malala
Mkutano huo uliotarajiwa kuwa wa kwanza kwa rais Goodluck Jonathan na wazazi hao pamoja na baadhi ya wasichana waliotoroka mikono ya boko haram, tangu Boko Haram kuwateka nyara wasichana zaidi ya mia mbili miezi mitatu iliyopita.
Wasichana hao walitekwanyara katika shule yao eneo la Chibok kazkazini mashariki mwa Nigeria.Mnamo siku ya Jumatatu mwanaharakati mdogo wa elimu Malala Yousafzai kutoka Pakistan alimsihi Rais Jonathan kukutana na wazazi wa wasichana hao.
Awali shirika la kimataifa la Human Rights Watch lilisema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa nchini Nigeria mwaka huu na wapiganaji wa kundi la Boko Haram.
Vifo hivyo vinaripotiwa kutokea katika mashambulizi yaliyofanywa katika zaidi ya miji sabini na vijiji Kaskazini mwa Nigeria.