Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe akizungumza na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa
ajili ya kuliombea Taifa yaliyofanyika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar
es Salaam. 


Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo
aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa
na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia
katika uvunjifu amani makanisani. 


Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika
Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki
ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na
Ubadhirifu wa mali za Kanisa. 


Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema
“Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi
itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari”.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu
ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam
katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. Maombi hayo yalifanyika katika
Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.