Tangu shambulizi la Westgate, harakati za kudhibiti ulinzi zimekuwa zikikosolewa
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limewalaumu polisi wa kupamba na ugaidi nchini Kenya kwa kufanya mauaji ya kiholela.
Human Rights Watch inasema kuwa pia imepata ushahidi wa watu kutoweka kwa lazima, kushikwa bila sababu na kudhulumiwa kwa washukiwa.
Shirika hilo pia linasema kuwa watoa misaada wa kimataifa wanastahili kusitisha misaada yao kwa polisi wa kupambana na na ugaidi kikosi kilichobuniwa baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa marekani mjini Nairobi mwaka 1998.