Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platinumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wake na kampuni inayoendesha programu ya Mziiki.Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Spice VAS Africa wanaoendesha programu hiyo ya Mziiki,Arun Nagar na kushoto ni Meneja wa Diamond Platinumz,Babu Talle.

Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki

kama Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa

kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika

walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa

mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.

"Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa Mziiki," anasema Arun

Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. "Kwa kushirikiana na

msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki.


Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu

na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na

kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani

pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki

streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. "