Mmoja wa wanaoshikiliwa
Raia watatu wenye asili ya Marekani,ambao wanashikiliwa Korea ya Kusini,wameongea na waandishi habari katika hali isiyokuwa ya kawaida,mahojiano yaliyoandaliwa na Pyongyang.
Raia hao ni Kennth Bae,jeffrey Fowle na Matthew Miller wameomba watumwe viongozi wa juu wa serikali ya marekani ili wakajadiliane kuachiliwa kwao.Wataalamu wa mambo wameyaongelea mahojiano hayo kua Korea ya Kusini inachohitaji ni kuyamaliza mambo na si vinginevyo.
Kati ya hao wanaoshikiliwa mmoja wao Bae , hali yake si nzuri na anahitaji matibabu ya haraka, ambaye anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela kwa jaribio la kwenda kinyume na sheria za Korea Kusini.
Nao Miller na Fowle wao wanasubiri hukumu yao kwa kile Korea Kusini walichokiita kuleta uhasama.
Serikali ya Marekani nayo ikajibu ya kwamba mateka hao waachiliwe mara moja chini ya haki za binaadamu.