Rais Dk. Jakaya Kikwete.
Na Haruni Sanchawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa upanuzi wa barabara ya Mwenge - Tegeta yenye urefu wa kilomita 12.9 Oktoba 1 mwaka huu katika eneo la Lugalo, njia panda ya Kawe jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Injinia Musa Lyombe amesema uzinduzi huo utafanyika kuanzia majira ya saa 4 asubuhi na kuongeza kuwa upanuzi huo ni mkakati wa serikali ya Tanzania kupunguza msaongamano katika Jiji la Dar es Salaam.