Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto)

akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH

inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean

(wa tatu kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa Kuuziana

Gesi kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Wengine katika

picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la

maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH

na MAUREL & PROM.

Wajumbe waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba gesi

katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na

MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele ni Waziri wa

Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na wawakilishi wengine

kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme

Tanzania (TANESCO).

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James

Andilile (wa kwanza kulia) wakipitia Mkataba kwa pamoja na mmoja wa

wawakilishi wa Kampuni hizo wakati wa kusaini Mkataba huo. Katikati ni

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MAUREL & PROM, Michael Hochard na wa

kwanza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH Robert MacBean.