Stori: Mayasa Mariwata
STAA asiyekauka kwenye vyombo vya habari Bongo, Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amesema kuwa, hawezi kujishughulisha kamwe na mgogoro uliopo kwenye Klabu ya Bongo Movie Unity unaomtaka mwenyekiti wao, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ ajiuzuru.Wema alifunguka alipokuwa akijibu swali lililomtaka aeleze mtazamo wake juu ya mgogoro huo ambapo alisema anatambua kwamba hali si shwari klabuni hapo huku baadhi ya wasanii wakidai mwenyekiti wao anachakachua fedha za chama lakini kwa upande wake hataki kujiingiza na ishu hiyo.
“Mh! Sio rahisi kabisa mimi kuingilia sekeseke hilo kusema eti Steve anafaa kuendelea na madaraka au kuachia ngazi, sitaki kuingilia hilo kabisa maana huwa sifuatiliagi sana mambo ya Bongo Movie zaidi ya vitu muhimu tu,” alisema Wema.