Tume ya Ulaya imeitaka Hispania kueleza ambavyo muuguzi huyo aliambukizwa Ebola na kuzua hofu ulaya

Tume ya Ulaya imeitaka Uhispania kueleza ambavyo muuguzi aliambukizwa Ebola mjini Madrid na kumfanya kuwa mtu wa kwanza kuambukizwa ugonjwa huo nchini humo kutoka Afrika Magharibi.
Muuguzi huyo ambaye amewekwa karantini alikuwa sehemu ya kukindi cha matabibu waliowatibu wamishonari wawili waliofariki kutokana na ugonjwa huo nchini humo.
Maafisa wa Afya nchini hispania wanasema kuwa muuguzi huyo anapokea matibabu.
Maafisa wakuu wanasema kuwa watu wnegine watatu wanachunguzwa hospitalini baada ya kushukiwa kuwa na dalili za Ebola. Watatu hao ni pamoja na mumewe muuguzi huyo , mfanyakazi mwingine wa afya na msafiri mmoja kutoka Afrika Magharibi.
Afisa mmoja wa afya nchini Hispania anasema kuwa muuguzi huyo angetengwa awali baada ya kugundulika kuwa na virusi hivyo.
Takriban watu 3,400 wamefariki kutokana na Ebola wengi wao wakiwa Afrika Magharibi.
Muuguzi huyo mwenye umri wa miaka 40,ambaye hajatajwa alikuwa anafanya kazi katika hospitali ya Carlos 111 mjini Madrid na alihusika katika juhudi za kuwatibu makasisi Maneul Garcia na Miguel Pajares waliofariki kutokana na Ebola.
Wote waliambukizwa Ebola wakiwa nchini Liberia katika shughuli za kimishionari.
Muuguzi huyo aliingia katika chumba alimokuwa mmoja wa wamishionari hao kumhuduumia na kusaficha chumba hicho baada ya kifo cha mmoja wao. Hata hivyo nyakati zote alipokuwa anafnya kazi yake alikuwa amevalia magwanda ya kujikinga kutokana na maambukizi
Maafisa wa afya wanasema hawajui chanzo cha maambukizi kwa muuguzi huyo maana alikuwa amevalia magwanda na hapoakuwa na taarifa za ajali yoyote iliyomuweka muuguzi huyo katika hatari ya kuambukizwa.