Wananchi wa Tanzania leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Rais wa kwanza na Baba wa Taifa hilo marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu alifariki nchini Uingereza alikokuwa amaelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Na kuzikwa katika kijijini cha Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania ambapo alizikwa Kiongozi huyo wa zamani na rais wa kwanza wa Tanzania.
wakati maadhimisho haya ya kitaifa yatafanyika mkoani Tabora, yakiambatana na kuzimwa kwa mwenge wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa la Tanzania wao wameadhimisha misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza zikiendelea, familia hiyo imesalia kijijini Mwitongo, na kudai kuwa siku hadi siku kumbukizi hiyo inapoteza maana.