Mwenyekiti wa African Stars Entertainment (ASET) Baraka Msiilwa wa Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake Bi Furaha Ramadhani Baraka (pichani akiwa na mdogo wake Omari Baraka), kilichotokea wikiendi hii mjini Liege,Ubelgiji.
 Mipango inafanywa kuurejesha mwili 

wa marehemu nyumbani kwa mazishi. 

Habari ziwafikie ndugu, jamaa, majirani na marafiki popote pale walipo.  Mola na aiweka roho ya marehemu mahali pema peponi

- Amina