Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.
Mji wa Barawe ulio umbali wa kilomita 200 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka sita.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.