Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014 

Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha 

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha