Polisi wa kenya (Picha na Maktaba).
Habari kutoka Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya zinasema kuwa, abiria 28 wameuawa na wengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia basi walimokuwa wakisafiria leo alfajiri.
Habari zaidi zinasema wavamizi hao huenda ni wanachama wa kundi la kigaidi la al-Shabab. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema wavamizi hao walikuwa wa asili ya kisomali na waliwaua abiria ambao si Waislamu. Jambo hilo linalenga kuzusha vita vya kidini nchini Kenya.
Ikiwa itathibitika kuwa al-shabab ndio waliohusika na hujuma hiyo,  hilo litakuwa shambulizi baya zaidi la kundi hilo kutokea katika miezi ya hivi karibuni. Polisi ya Kenya imekataa kutoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na kusisitiza kuwa, itatoa maelezo punde baada ya kuchunguza kadhia hiyo.