Kufuatia mkutano wa Watanzania waishio ujerumani na Rais wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete, Mweyekiti wa umoja wa watanzania Ujerumani UTU e.V Bw, Mfundo Peter Mfundo ameeleza matarajio ya Watanzania waishio Ujerumani, alifafanua kwamba japokuwa Rais Kikwete amebakisha muda mfupi katika uongozi wake lakini Umoja huo unaamini kuwa madam Rais Kikwete ameona umuhimu wa kufanya mkutano na Watanzania wanaoishi ujerumani basi anaweza akatekeleza  mahitaji ya Watanzania hao, Bw Mfundo alifafanua pia  hoja za msingi ambazo zitaibuka kwenye mkutano huo ni pamoja na Utekelezwaji wa upatikianaji wa fursa zilizopo Tanzania kwa watanzania wanaoishi Ujermani,(Diaspora) aidha aliendelea kueleza kwamba hoja nyingine ya msingi ni kutaka kujua msimamo wa serikali juu ya Uraia Pacha, kwani Watanzania wanaoishi ujerumani wana kiu kubwa ya kujua swala la Uraia pacha limefikia wapi. akiendelea kuongea na Mtangazaji Grace Kabogo kupitia sauti ya Radio Deutsche Welle idhaa ya kiswahili Bw. Mfundo alisema kutokana na Vijana wengi wa Tanzania kujiajiri kupitia Muziki  na kuupiga vita umasikini, Umoja wa Watanzania Ujerumani Utamuomba rais Kikwete kusaidia kupitisha msamaha wa kodi kwa Vyombo vya Muziki ili kuwawezesha Vijana wa Tanzania kumudu ununuzi wa vifaa hivyo, Bw. Mfundo alieleza moja ya changamoto wanazozipata  ni pale umoja huo unapokosa mawasiliano ya moja kwa moja na Idara ya Diaspora Tanzania.