Kanisa lisilo Rasmi Lavunjwa Kawe
Kanisa la lisilo rasmi la mchungaji ngwajima  lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja vya Tanganyika Packers  Kawe, limeamuriwa kuondoka mara moja  na ku
wacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya watu wa kawe. Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu  lemekuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.  Katika Barua iliosainiwa na Meneja wa Mkoa wa kinondoni wa shirika la nyumba  la Taifa  imesisitiza kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha  shughuli zake lakini shirika hilo  halitaweza kutoa ruhusa  kwa  kanisa hilo kuendelea kufanya  mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo limeshaanza  kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE ikiwa ni ujenzi wa makazi  n.k  Bw Masika ametoa siku 30 tu  ili Mchungaji Ngwajima kujitayarisha na kuwacha viwanja hivyo wazi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.