Na Mussa Mateja

HATIMAYE siri ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuhamia kwenye mjengo wake wa kisasa uliyopo Tegeta -Madale jijini Dar imevuja huku ikitajwa kuwepo na vionjo vya ushirikina.
Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Chanzo makini kimeliambia Amani kuwa, licha ya kumalizika kwa mjengo huo, lakini Diamond alikuwa akikataa kuhamia kutokana na umbali kutoka huko hadi mitaa aliyoizoea lakini shinikizo lilikuja kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Zarina Hassan ‘Zari’  ambaye tangu aliponasa ujauzito amekuwa akitamani kuwa karibu na mpenzi wake huyo ila ilikuwa ikishindikana kufuatia mazingira aliyokuwa akiishi mwanzo Diamond, Sinza-Mori, Dar.
Muonekano wa mjengo wa  Diamond.
“Ndugu yangu kama unataka kufahamu undani zaidi wa hiki ninachokueleza muulize Diamond mwenyewe atakwambia, Zari siku zote alikuwa akitaka kuwa karibu na Diamond, hasa baada ya ujauzito lakini ndugu zake walikuwa wakimkatalia kufanya hivyo kwa kuhofia mimba yake kuchoropoka kutokana na vijicho vya watu.
zari 10
Mpenzi wa Diamond Platinumz, Zarina Hassan ‘Zari’ akiwa katika mjengo huo.
“Kingine kilichokuwa kikimfanya Diamond ashindwe kumruhusu Zari kuwepo makazi ya awali ya Diamond ni mama yake alipougua, si unajua ilidaiwa yalikuwa ni mambo ya kishirikina?“Amini usiamini kutokana na mambo hayo, ilibidi Zari amwambie Diamond akamilishe nyumba yake haraka iwezekanavyo ili tu aweze kuhamia na yeye aje kukaa maana tangu awe mjamzito mara kadhaa amekuwa akitamani sana kuishi na Diamond,” kilisema chanzo hicho.
Juzi, paparazi wetu alimtafuta Diamond laivu ili aweze kuyaweka sawa madai hayo ambapo baada ya kupatikana alijibu hivi:“Kaka, hayo maneno wewe achana nayo maana kila mtu anaongea anachokifahamu, isitoshe yanaongewa mengi kwa kuwa wanajua nimehama Sinza. Ila ninachoweza kusema kila jambo linapangwa na Mungu hivyo sina uwezo wa kuwazuia watu kusema wanachojisikia.”
Jumamosi iliyopita, Diamond alikata shauri na kuhamia kwenye makazi yake mwenyewe baada ya ujenzi wa miaka karibia mitatu. Kwa mujibu wa mkandarasi mmoja, nyumba hiyo mpaka kukamilika kwake, imetafuna karibu shilingi milioni mia nne (400,000,000).