Ufisadi:Kenyatta awasimamisha kazi maafisa wakuu serikalini 175 kufuatia tuhuma za ufisadi dhi yao
Mawaziri 5, makatibu 6 wa kudumu na Magavana 10 wametajwa miongoni mwa maafisa 175 wa umma watakaolazimika kunga'atuka
mamlakani katika siku 60 zijazo iliuchunguzi wa kina ufanyike kuhusu madai ya ufisadi dhidi yao.
Hayo yalibainika katika ripoti iliyotolewa bungeni na rais Uhuru Kenyatta katika kikao maalum cha bunge la taifa kilichowajumuisha wabunge na maseneta.

Rais Kenyatta aliwataka maafisa wote wa umma waliotajwa katika ripoti hiyo waondoke ilituhuma zote dhidi yao zichunguzwe kwa kina na tume ya kupambana na ufisadi.
''Kwa hakika imewadia wakati ambapo serikali yangu haina budi ila kuchukua hatua mahsusi ambayo inalenga kukomesha hili zimwi la ufisadi mara moja''
UFISADI ''Ufisadi umevuka mipaka na lazima nasi tujifunge kibwebwe na kukabiliana nao''.
''Natarajia kuwa wale waliotajwa katika ripoti hii watanga'tuka mamlakani hadi pale uchunguzi utakapokamilishwa ndipo warejee afisini.'' alisema Kenyatta.
Kenyatta aliongezea kusema kuwa ''Ninamtaka kiongozi wa mashtaka ya umma kuanzisha uchunguzi mara moja kuhusiana visa vyote vilivyotajwa humu katika kipindi cha siku 60 zijazo''.
Ripoti hiyo iliyotayarishwa na tume ya kupambana na ufisadi nchini Kenya KACC inawadia wakati ambao kumekuwa na visa vingi vya ufisadi haswa katika serikali kuu na pia serikali za majimbo.
Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kisa kilichozua mjadala ni kile cha 'Anglo Leasing'' ambayo ilijumuisha kandarasi za idara ya Uhamiaji idara ya upelelezi na Idara ya usalama wa taifa.
Mabilioni ya fedha yalilipwa kwa wanakandarasi waliotarajiwa kuwasilisha kazi ambazo hazikuwahi kufanyika hata wa leo.
Magavana 10 kati ya 47 wametajwa katika ripoti hiyo ambayo itatangwwa rasmi siku ya jumanne katika mabunge yote mawili.
Duru zinasema kuwa Kamati nzima ya bunge inayochunguza ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma imetajwa katika ripoti hiyo.
MSAMAHA
Aidha Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Kenyatta alisema''ili wakenya waweze kusonga mbele na kusahau yaliyopita kufuatia hatua zilizochukuliwa na serikali zilizotangulia ni wajibu wangu
kuchukua fursa hii na kuwaomba msamaha wote waliodhulumiwa kwa njia moja au nyengine.
Rais Kenyatta aliwaomba radhi maelfu ya wakenya waliohujumiwa na serikali zilizotangulia.
Zaidi ya Wakenya 650,000 walifukuzwa makwao kufuatia vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2008 na tume maalum ya haki ukweli na maridhiano TJRC
ilipendekeza kuwa sharti serikali iombe radhi kwani fedha haziwezi kufuta machungu ya mateso ambayo wakenya wamepitia''
''Hata hivyo licha ya mapendekezo ya tume hiyo ya maridhiano,nimeagiza wizara ya fedha itenge shilingi bilioni 10 dola milioni 110, katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo kwa ajili ya kuwafidia wale wote walioathirika''