Waandamanaji Afrika Kusini
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma ameahirisha ziara yake ya ughaibuni kutokana na hali ya ghasia za kibaguzi dhidi ya wageni katika taifa lake.
Alitarajiwa kuhudhuria mkutano nchini Indonesia. Rais Zuma ambaye amekosolewa kwa kushindwa kuonyesha uongozi anatarajiwa kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Chatsworth mjini Durban.
Polisi nchini Afrika Kusini wamewaagiza raia kutotuma ujumbe usiothibitishwa kuhusu mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni kwa sababu hatua hiyo inazua hofu.

Polisi wanesema kuwa kuna wasiwasi kuwa uvumi huo unachochea ghasia dhdi ya wahamiaji.
Maafisa wa polisi wakikabiliana na waandamanaji Afrika Kusini
Watu 30 waliakamatwa wakati wa ghasia za usiku kucha mjini Johannesburg.
Biashara kadha zinazomilikiwa na raia wa kigeni ziliharibiwa.
Takriban watu watano wameuawa kwenye mashambulizi yaliyaonza baada mfalme wa kizulu Goodwill Zwelethini kusema kuwa wageni wanahitajka kuondoka Afrika Kusini.