Wapiganaji wa kisunni waliojitolea nchini Iraq
Vikosi vinavyoitii serikali ya Iraq vimelishambulia kundi la wapiganaji la Islamic State katika eneo la Ramadi kwa mara ya kwanza tangu mji huo utekwe wiki moja iliopita.
Maafisa wanasema kuwa vikosi hivyo vya usalama na wapiganaji wa kishia wamewafurusha wapiganaji wa IS kutoka mji wa Hussaiba ,kilomita kadhaa mashariki mwa mji wa Ramadi.

Wakati huohuo muungano wa majeshi unoongozwa na Marekani umekuwa ukiwashambulia wapiganaji wa IS kutoka hewani.
Wanajeshi wa serikali nchini Iraq
Waandishi wanasema kuwa kuna wasiwasi kwamba kupelekewa kwa waipiganaji wa kishia katika jimbo la waislamu wa Sunni huenda kukazua mvutano wa kidini.
Lakini vikosi vya usalama vilifurushwa vibaya katika eneo la Ramadi swala linalosababisha serikali kuwategemea sana wapiganaji wa kishia ili kuweza kuuchukua mji huo