Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo[jana] mjini Dodoma huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika wa Bunge hilo Mh.Anna Makinda wakisikiliza.
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo[jana] huku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Spika Mhe.Anna Makinda wakishuhudia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi wakati Rais huyo wa Msumbiji alipowasili katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma na kuzungumza na viongozi waandamizi. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Bwana Mwigulu Nchemba.
(Picha na Freddy Maro)