Wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania
Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya visa 400 vya ugonja wa kipindupindu vinaripotiwa kila siku miongoni mwa wakimbizi wa Burundi walio nchini Tanzania.
Maelfu ya watu wamewasili kwa mashua wakikimbia ghasia za kisiasa nchini Burundi
Wamechukua hifadhi katika sehemu zenye misongamano na zilizo na mazingira mabaya.
Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban watu 3000 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu na hadi sasa zaidi ya 30 wameaga dunia.
Maandamano yanaendelea kwenye mji mkuu wa Burundi, Bujumbura kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu