Image copyright.
Image captionGoogle yaamua kwenda na kasi ya uhitaji wa huduma ya watumiaji wake
Google imebadili nembo yake mpya kwa ajili ya watumiaji wake
mwonekano mpya wa nembo hii unaonekana kuwa wa rangi zenye kuvutia.
Google imesema mabadiliko haya yalihitajika kwa sababu watumiaji wake wengi wanapatikana kwenye simu za mkononi kuliko Kompyuta za mezani.
kampuni ya Google imesema muonekano wa Nembo hii mpya, ni mzuri kwenye vioo vya aina mbalimbali vya simu na vifaa vingine ambavyo watumiaji wake hutumia Google
Google imetangaza mabadiliko ya mtandao wake wakisifu kuwa ni rahisi zaidi,yenye kupendeza,ya kirafiki nembo ya sasa ya Google imepambwa kwa rangi ya blue,nyekundu,njano na kijani.