kingunge
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Mwanasiasa mkongwe nchini ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngombale Mwiru hivi punde wakati akiongea na wanahabari jijini Dar ametangaza kuachana na chama hicho maana kimeshindwa kuheshimu katiba yake.
Mzee Kingunge amesema hajiungi na chama chochote ila yupo upande wa mabadiliko.
Mzee Kingunge alijiunga na TANU mwaka 1954 akiwa mwanachama wa saba tangu chama hicho kuanzishwa.