Image copyrightepa
Image captionKuna shinikizo linaloongezeka la kisiasa kwa kansela wa nchi hiyo kukoma kuwapokea wakimbizi.
Wakimbizi milioni moja u nusu wanatarajiwa kutafuta hifadhi nchini Ujerumani mwaka huu kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari.
Makadirio hayo mapya ambayo hayajathibitishwa na serikali ya Ujerumani yanajiri wakati kuna ongezeko la wasiwasi kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabilianana idadi kubwa kama hiyo ya wakimbizi na .
Serikali ya Ujerumani inakadiria watu laki nane watatafuta hifadhi huko mwaka huu licha ya kuwa baadhi ya wanasiasa wameonya huenda idadi hiyo ikaongezeka maradufu.
Image copyrightReuters
Image captionWasiwasi unaoongezeka kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabiliana na hilo.
Sasa duru zilizonukuliwa katika gazeti moja la Ujerumani inadai wakimbizi na wahamiaji milioni moja na nusu watawasili mwaka huu.
Kiwango ambacho ni maradufu ya kadirio lililotolewa awali.
Image copyrightGetty
Image captionUjerumani kupokea wakimbizi milioni 1.5
Wasiwasi unaoongezeka kuhusu uwezo wa Ujerumani kukabiliana na hilo.
Jana maelfu ya watu walijumuika katika maandamano ya kupinga wakimbizi katika baadhi ya miji Ujerumani.
Image copyrightGetty Images
Image captionSerikali ya Ujerumani inakadiria watu laki nane watatafuta hifadhi huko
Na kuna shinikizo linaloongezeka la kisiasa kwa kansela wa nchi hiyo kukoma kuwapokea wakimbizi.
Lakini, Angela Merkel anaendelea kutetea sera yake ya kuruhusu wakimbizi hao akisisitiza nchi hiyo ina uwezo wa kukabiliana na hali iliyopo.