FREDRICK MWAKALEBELA AKIWA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM  WILAYA YA IRINGA MJINI WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.

 BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOANI IRINGA WALIPOKUWA WANAWASIKILIZA FREDRICK MWAKALEBELA NA ELISHA MWAMPASHE KATIBU WA CCM WILAYA YA IRINGA MJINI.





Chama cha mapinduzi wilaya ya iringa mjini
kimekanusha kufutwa kwa kesi yao dhidi ya mkurungenzi wa manispaa hii pamoja na
mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji PETTER MSINGWA.


akizungumza na waandishi wa habari katibu wa ccm
wilaya ya iringa mjini ELISHA MWAMPASHE amesema kuwa taarifa zilizosambaa
sehemu mbalimbali sio za kweli.

“Nimekuwa nikipigiwa simu nyingi toka jana nikipewa
taarifa kuwa kesi yetu imetupiliwa mbali na imeenea sana kwenye mitandao ya
kijamii na maeneo mbalimbali ukweli ni kwamba kesi ya uchaguzi namba tano ya
2015 haijafutwa”alisema Elisha mwampashe.

Mwampashe ameongeza kuwa kesi hiyo bado haijapangiwa
siku ya kusikilizwa wala kupangiwa jaji wa kuendesha kesi hiyo hivyo anashangaa
kuaona taarifa zinazendelea kuenena mitaani

“Ifahamike kuwa mahakamani kuna shauri la
msingi  ambalo lilikuwa na kupinga
matokeo na kuna  shauri dogo  namba 28 la mwaka 2015 ndio lilikuwa
likizungumziwa jana kwa lengo la kuomba kupunguziwa dhamana kutokana na sheria
kuruhusu kufanya hivyo” alisema Elisha mwampashe.

Mwampashe amemalizia kwa kuwataka wananchi  na wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea
kuwa na subra kwa kuwa haki yao ya msingi itapatikana mahakani na kuwasii
wananchi wanaopotosha taarifa hizi.

 kwa upande
wake fredrick mwakalebela aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini
amesema kuwa shauri lilofutwa ni la kuomba kupunguziwa pesa ya dhamana.

“Nilikuwa kimya kutokana na kufatilia swala hili
kimya kimya kwa lengo la kupata haki yangu ya msingi ambayo nimenyang’anywa na mkurugezi
wa manispaa ya iringa pamoja na mchungaji petter msingwa” alisema Fredrick
mwakalebela 

Mwakalebela amemalizia  kwa kusema kuwa kesi hiyo inaendeshwa naye
pamoja na chama cha mapinduzi kwa kuwa chama ndio kilichompa nafasi ya kugombea
ndio maana kila kitu anachokifanya chma lazima kijue juu ya kesi hivyo. 

ilitolewa
taarifa Kuhusu kutupiliwa mbali kwa shauri ya dhamana ya kesi ya ubunge Iringa
Mjini Msajiri wa Mahakama kuu Iringa Bi Ruth Masamu amesema kesi ya aliyekuwa
mgombea ubunge Jimbo La Iringa Mjini Fredrick Mwakalebela alitoa ombi la kuomba
kupunguziwa dhamana kutoka milioni kumi na kushuka angalau kwa kiasi kidogo.




Hii ni
kutokana na vifungu vya sheria kuruhusu kuomba ombi hilo na mahakama kulikataa
na kumtaka aongeze mtuhumiwa ambaye ni mwanasheria wa serikali kwenye kesi yake
kwa gharama hiyohiyo.






Hivyo uvumi
uliotolewa jana kwamba kesi imefutwa si kweli kwa sababu mpaka sasa kesi bado
haijapangwa wala kuanza kusikilizwa.