Watu wanne wameuawa katika shambulizi la guruneti mjini Bujumbura Burundi katika baa moja.
Waathirika ni pamoja na mtoto ambaye alikuwa akiuza mayai ya kuchemshwa.
Hakuna aliyekiri kutekeleza shambulizi hilo .

Siku ya Ijumaa, kikundi cha waasi cha FOREBU kilikiri ndicho kilichokuwa kikifanya mashambulizi kadhaa ambayo watu watano waliuawa - baadhi yao maafisa wa usalama .
Image copyrightbbc
Image captionFOREBU kilikiri ndicho kilichokuwa kikifanya mashambulizi kadhaa ambayo watu watano waliuawa
Watu mia 400 wamekufa katika mashambulizi na maandamano tangu Aprili, Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza nia ya kuwania muhula wake wa tatu uongozini.
Umoja wa Afrika unajaribu kumshawishi rais Nkurunziza kukubaliana na kupelekwa kwa askari wa kulinda amani AU , nchini humo lakini yeye alikataa.