Mamilioni ya watu wenye asili ya China, duniani kote wanasheherekea mwaka mpya wa ki China .
Baruti nyingi zilirushwa angani mjini Beijing ikiwa ni ishara ya kusheherekea siku ya kwanza ya mwaka mpya wa nyani,Nyani wakiwa ni miongoni mwa wanyama kumi na mbili wanaotumiwa kati ya alama za kichina katika masuala ya utabiri.

Nako mjini Yokohama nchini Japan, wao wanasheherekea siku kuu hii kwa kuhesabu muda huku wakicheza ngoma ya asili ya kucheza na simba.
Maadhimisho ya sherehe hizi za mwaka mpya zinajumuisha watu kula pamoja,kufanya usafi na familia kuwa pamoja huku wakirusha fashi fashi angani.