Serikali ya Tanzania imewahakikishia wakaazi wa jiji la Dar es Salaam kwamba inatatua tatizo la uhaba wa maji mjini humo na hivi karibuni tatizo hilo litakuwa historia.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania,naibu waziri wa maji na unyunyizaji Bw Issack Kamwelwe amesema kuwa serikali kwa sasa imeanzisha mradi wa kuimarisha usambazaji wa maji katika maeneo ya mji yanayokumbwa na uhaba mkubwa wa maji.

Kulingana na Bw Kamwele,mradi huo ambao una thamani ya dola milioni 32.9 na na unaotarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka 2017 unashirikisha kubadilisha mabomba ya zamani,na kuweka mapya na kuweka mabomba mapya maeneo ambayo hayajaangaziwa.
Baadhi ya maeneo ambayo yatafaidika na mradi huo ni mji wa bagamoyo,Mpiji,Bunju,Mabwepande,Boko,Bweni,Tegeta,Ununio,Wazo,Salasala, Kizundi,matosa,Mbezi juu,Goba,Changabyikeni,makongo,Kiluvya,Kibamba,Mbezi,Msakuzi,Mkabe,Maramba Mawili na Msigali.