Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw.
Moses Hella, akielezea moja kati ya gunduzi za kampuni yake kwa wageni
(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka minne ya Chinese Alumni
Association.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec Limited, Bw. Moses Hella (kulia) akielezea moja kati ya gunduzi ya kampuni yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Profesa Elisante Ole Gabriel (Wapili Kulia) wakati wa hafla ya kuazimisha miaka mine ya Chinese Alumni Association nchini hivi .

Dar es Salaam, Julai 4, 2016. Kampuni mpya ya masuala ya TEHAMA nchini
Tanzania, Emotec Limited yaeleza kuwa imejizatiti katika kutoa huduma bora na zenye
ubunifu wa hali ya juu kwa wateja wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Emotec, Bw.
Mosses Hella imesema kuwa kampuni yake ina mpango wa kuwa inayoongoza katika
utoaji wa huduma na bidhaa bora katika soko la TEHAMA nchini.
“Tumedhamiria kutoa bidhaa za gharama
nafuu, huduma bora, za kibunifu na suluhisho kwa wateja wetu. Lengo letu kuu ni
kuwa kampuni yenye ubunifu zaidi iliyojizatiti katika utoaji wa huduma bora na
za gharama nafuu katika mausuala ya TEHAMA nchini.” Alisema Bw. Hella
Bw. Hella amesisitiza kuwa kampuni
yake pia inayo dhamira ya kubuni, kutengeneza, kusambaza na kufanyia
marekebisho vifaa mbalimbali vya umeme hususani simu za mkononi, tablet,
kompyuta, router na modemu za intaneti pamoja na luninga ambapo wamejikita
zaidi katika ubora.
Mbali na hayo aliongezea kuwa
Emotec ni kampuni ya masuala ya TEHAMA inayotazamia pia kutoa huduma za vitabu
kwa njia ya mtandao (e-content) katika kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu
nchini.
“Pia tunawekeza katika kubuni na
kuchapisha vitabu kwa njia ya mtandao (e-content) kwa ngazi za elimu ya shule
ya msingi, sekondari na ya juu ili kusaidia kuimarisha mfumo wa elimu nchini.”
Alibainisha
Aliongezea pia shughuli nyingine
ambazo kampuni yake inajihusisha nazo ni pamoja na kubuni, kufunga na kusaidia
Maabara ya Usimamizi wa Mifumo wa Taarifa, Mifumo ya Usimamizi wa Mapato,
Mifumo ya Usimamizi wa Taarifa za Shule, Mifumo ya Usimamizi ya Hoteli na
mifumo ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao.
Kwa kuongezea zaidi kampuni pia
imewekeza katika kubuni, kufunga na kusaidia mifumo midogo ya fedha na program
tanzu ya kibenki lakini pia ina mfumo mzuri wa kimtandao kwa bandari, viwanja
vya ndege na vituo vya makontena.


“Hivyo basi ningependa kuchukua
fursa hii kuwaalika watanzania kutembelea banda letu katika maonyesho ya 40 ya
kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo tunaonyesha
bidhaa zentu zenye ubinifu na tekinolojia ya kisasa kabisa kwani hapo ndipo
mahali wanapoweza kujua mengi zaidi kuhusu kampuni yetu.” Alihitimisha Bw.
Hella