Waumini wa dini ya Kiislam wa kitongoji cha Mol nchini Ubelgiji wakipata picha ya pamoja mara baada ya salat Eid mapema leo asubuhi

Baada ya mwezi mzima wa mfungo mtukufu wa Ramadhani leo imekuwa ni furaha kwa waislam wote duniani kwa kusheherekea sikukuu ya Eid el Fitr pamoja,pichani ni baadhi ya waumini wa Kiislam kitongoji cha Mol nchini Ubelgiji
Kila penye heri huwa na Amani na kila penye Amani huwa na heri,pichani Maganga One Blogger,Askali polisi wa Mol na wana Mol wakiwa na furaha kuhakikishiwa usalama katika sikukuu ya Eid kitongojini mwao.

Maganga One Blog inawatakia kila la heri na baraka tele kwa waislam wote duniani,tufurahie sikukuu yetu kwa kula vizuri,kuvaa vizuri, kutembeleana,kuwaona wagonjwa mahospitali,kuzulu makaburini na kupeana mikono ya furaha.